Waasi watoa masharti yao nchini Libya

Mwanajeshi wa waasi nchini Libya. Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanajeshi wa waasi nchini Libya.

Wanajeshi wa waasi nchini Libya, wanasema wako tayari kusitisha mapigano ikiwa kiongozi wa taifa hilo Kanali MuamMar Gadaffi atayaondoa wanajeshi wake katika miji mikuu nchini humo na kuruhusu maandamano ya amani.

Lakini kiongozi waasi hao Mustafa Abdel Jalil, ambaye pia kaimu kiongozi la baraza la upinzani amesema kwamba kamwe hawawezi kulegeza msimamo wao wa kumtaka Bwana Gadaffi kujiuzulu.

Huku mapigano yakiendelea, ripoti zinasema, wanajeshi watiifu kwa serikali wanaendelea kushambulia mji unaothibitiwa na upinza wa Misrata kwa mabomu.

Wakati huo huo, daktari mmoja mjini humo ameiambia BBC kuwa raia 7 waliuawa kwenye shambualio la anga lililolenga msafara wa magari ya serikali.

Lakini madai hayo hayajathibitishwa rasmi.