Blackburn yaibana Arsenal

Arsenal imeshindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 na Blackburn Rovers.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal imebanwa na Rovers

Licha ya Blackburn kucheza kwa karibu dakika 15 za mwisho wakiwa wachezaji 10, Arsenal walishindwa kutumia mwanya huo kujipatia ushindi.

Steven Nzonzi wa Blackburn alioneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Laurent Koscielny.

Matokeo hayo yanaiacha Arsenal katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 59. Kwa Blackburn sare hiyo ni njema kwao wakiwa na pointi 34 katika nafasi ya 14.