Uchaguzi Nigeria Unaahirishwa

Kumezuka hamasa katika vituo vya kupigia kura nchini Nigeria, baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, kutangaza kuwa uchaguzi wa wabunge wa leo, umeahirishwa hadi Jumatatu

Profesa Attahiru Jega alisema uamuzi huo ni wa dharura, kwa sababu ya matatizo ya uratibu.

Upigaji kura ulikuwa umeanza, na watu wengi walijitokeza katika miji kama Lagos na Kano.

Mwandishi wa BBC mjini Lagos, anasema maswala sasa yanaulizwa kuhusu uwezo wa Profesa Jega na hatima yake.

Bi Jega anasema, alisema kuahirishwa huko ni pigo kubwa kwa Nigeria, ambayo ikijaribu kusahau historia ya chaguzi zenye dosari.