Duekoue Bado Hakujatulia

Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, kinasema kinajaribu kuwalinda maelfu ya raia waliojificha kwenye kanisa, mjini Duekoue, magharibi mwa nchi, ambako watu kama mia nane waliuwawa juma lilopita.

Mwandishi wa BBC mjini Duekoue, anasema bado hakujatulia.

Anasema aliona wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu, wakiondosha maiti na kuwazika kwa pamoja.

Wakati wa mauaji makubwa, eneo hilo lilikuwa likidhibitiwa na wafuasi wa Alassane Ouattara, ambaye anatambuliwa kimataifa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa mwaka jana.

Amesema kuwa wapiganaji wake hawakuhusika.