Tutu Anataka Vita Vimalizwe Libya

Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, ametoa wito kwa vita vya Libya kumalizwa haraka, hata ikimaanisha kuwa Kanali Gaddafi apewe hifadhi na nchi nyengine.

Akizungumza na BBC, Askofu Tutu alisema kimsingi kiongozi wa Libya angelifaa kufikishwa mahakamani, lakini ukweli halisi ni kuwa bora kumpa hifadhi, ili kunusuru maisha ya watu.

Afrika Kusini ilipiga kura kuunga mkono azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuingilia kati kijeshi, lakini hivi karibuni imelalamika juu ya mashambulio ya ndege ya jeshi la kimataifa.

Viongozi wa ukombozi wa Afrika Kusini, pamoja na Nelson Mandela, waliungwa mkono sana na Colonel Gaddafi.