Mashambulio Gaza

Mapigano yameendelea kwa siku ya tatu katika eneo la Gaza, katika mapambano makali kabisa tangu Israel kushambulia Gaza, Januari, mwaka wa 2009.

Wakuu wa Israel wanasema makombora kama 20 yamelengwa dhidi ya eneo la kusini la Israel ; na Israel imefanya mashambulio zaidi ya ndege huko Gaza, kulipiza kisasi.

Wapiganaji watatu wa Hamas walikufa katika shambulio moja la jana usiku; na kufikisha jumla ya Wapalestina waliouwawa tangu Alkhamisi, kuwa 17.

Mashambulio yalizuka baada ya kombora kupiga basi la shule la Israel na kujeruhi watu wawili.