Fujo zimezuka tena Burkina Faso

Kumetokea fujo nyengine nchini Burkina Faso.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Inaarifiwa kuwa wanajeshi wanaolalamika juu ya malipo na mafao wamepora maduka na vibanda vya sokoni katika mji mkuu, Ouagadougo.

Mamia ya wenye maduka waliokuwa na hasira walijibu kwa kushambulia ofisi ya baraza la jiji na kuchoma moto makao makuu ya chama tawala.

Inasemekana ghasia hizo zinaendelea.

Siku ya Ijumaa, Rais Blaise Compaore, alifuta baraza lake la mawaziri na kumteua mkuu mpya wa jeshi, ili kurejesha udhibiti wa serikali yake.