Jeshi linashambulia Ajdabiya na Misrata

Taarifa kutoka Libya zinaeleza kuwa jeshi la Kanali Gaddafi, limekuwa likishambulia kwa mizinga mji wa Ajdabiya unaodhibitiwa na wapiganaji.

Haki miliki ya picha Getty Images

Walioshuhudia mashambulio hayo wanasema makombora zaidi ya 10 yalipiga karibu na mitaa ya magharibi ya mji huo, na kufanya wapiganaji wakimbie.

Baadhi ya taarifa zinasema jeshi la Kanali Gaddafi linakaribia Ajdabiya. Piya kulikuwa na ripoti kwamba jeshi hilo limeanza tena kushambulia kwa mabomu, mji wa Misrata, ulioko magharibi mwa nchi.

Msemaji wa upinzani alieleza kuwa watu 6 waliuwawa huko mapema hii leo.