Goodluck anaongoza sasa

Matokeo kutoka karibu nusu ya mikoa 36 ya Nigeria yanaonesha kuwa rais wa sasa, Goodluck Jonathan, anaongoza katika uchaguzi wa rais.

Haki miliki ya picha Reuters

Bwana Jonathan, Mkristo kutoka eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta, hadi sasa ana kura mara mbili zaidi kwa wingi kushinda mpinzani wake mkuu, kiongozi wa zamani wa kijeshi, Muhammadu Buhari, ambaye amepata kura nyingi eneo la kaskazini lenye Waislamu wengi.

Waandishi wa habari wanasema, ikiwa mtindo wa sasa utaendelea, Rais Jonathan ataweza kushinda katika duru hii ya kwanza.

Wasimamizi kutoka nchi za nje wanasema, uchaguzi wa Jumamosi unaweza kuwa wa mwanzo kuaminika, tofauti na chaguzi za miongo kadha ambazo zilikuwa na udanganyifu na ghasia.