Vyama vya upinzani vinang'ara Nigeria

Ishara za awali kutoka uchaguzi wa wabunge wa Nigeria, zinaonesha kuwa chama tawala cha PDP kimepoteza viti kadha katika maeneo ambako kilikuwa na nguvu.

Huku kura zinahesabiwa, vyama vipya vya Congress for Progressive Change, na Action Congress of Nigeria, vimepata kura.

Wakati wa upigaji kura Jumamosi, kulizuka ghasia, ambapo mabomu mawili yaliripuka kwenye vituo vya kupigia kura katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi, ambako piya mawanasiasa mmoja wa huko alipigwa risasi na kuuwawa.

Matokeo yote ya uchaguzi yanatarajiwa kuwa tayari saa 48 baada ya upigaji kura.