Makabila hayataki vita Misrata, Libya

Serikali ya Libya imeonya kuwa makabila yanayomuunga mkono Kanali Gaddafi huenda yakaingia kwenye vita dhidi ya wapiganaji mjini Misrata, hatua ambayo inaweza kupelekea damu zaidi kumwagika mjini humo.

Waziri Mdogo wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Libya, Khaled Kaim, alisema makabila ya eneo la Misrata yamelipa jeshi la Libya shuruti..kwamba jeshi limalize mapigano mjini Misrata, ama sivyo, makabila hayo yataingilia kati, kupambana na wapiganaji hao.

Waziri huyo huyo alisema makabila yamekerwa kuwa maisha yao yamechafuliwa na mapigano ya Misrata, ambayo yamekuwa yakiendelea tangu mwezi wa Februari.

Barabara kuu haipitiki, na biashara mjini Misrata imesimama.

Kawaida, mji wa Misrata ni pahala pa biashara nyingi, na bandari yake ni ya pili kwa ukubwa, baada ile ya Tripoli.

Waziri Khaled Kaim alisema jeshi limetumia busara mjini Misrata, ili kupunguza muaji ya raia.

Alionya kuwa makabila hayatochokua tahadhari hiyo.