Mwaliko wa harusi unatangazwa

Maelezo zaidi yametolewa kuhusu orodha ya watu walioalikwa harusi ya juma lijalo, ya mjukuu wa malkia wa Uingereza, Prince William, na Kate Middleton.

Haki miliki ya picha AFP

Watu 46 kutoka familia nyengine za kifalme za nchi za ng'ambo wamealikwa.

Kati yao ni Prince anayetawala Bahrain na Mfalme wa Swaziland - ambao kuhudhuria kwao kutakuwa swala tete kidiplomasia, kwa sababu nchi zote mbili zimekandamiza maandamano dhidi ya serikali.

Kati ya wageni mashuhuri walioalikwa ni mwimbaji Elton John, mcheza mpira David Beckham, na mchezaji wa sinema, Rowan Atkinson.

Jamaa wa wanajeshi wa Uingereza waliouwawa nchini Iraq na Afghanistan, piya wamo kwenye orodha.