Mapigano Sudan Kusini

Wakuu wa Sudan Kusini wanasema maelfu ya raia wamekimbia mapigano makali baina ya wapiganaji na jeshi la serikali ya Sudan Kusini, katika eneo muhimu la mafuta.

Haki miliki ya picha BBC World Service Trust

Wafanyakazi katika sekta ya mafuta wamehamishwa kutoka eneo hilo.

Makundi kadha ya wapiganaji yanapigana na serikali ya Sudan Kusini, yakiiishutumu kula rushwa.

Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya 800 wameuwawa, na karibu laki moja wamehama makwao tangu mwezi Januari, wakati Sudan Kusini ilipopiga kura kuamua kuwa inataka kujitenga na Sudan Kaskazini.