Gbagbo akamatwa Ivory Coast

Habari za hivi punde zinaelezea kwamba vikosi maalum vya Ufaransa vimefanikiwa kuingia Ivory Coast na kumkamata Bw Lauren Gbagbo, ambaye amekuwa akikataa kuondoka marakani na kumuachia madaraka ya urais mpinzani wake Alassane Ouattara.

Awali kulikuwa na shughuli ya wanajeshi wa Ufaransa kuingia katikati ya mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan.

Wakiimarisha juhudi zao kwa kutumia magari ya deraya na helikopta za kijeshi, walielekea kwa kasri ya Laurent Gbagbo.

Kulikuwa na taarifa za awali kwamba Bw Gbagbo alikuwa amejificha katika mahandaki ya chini kwa chini katika kasri hiyo.

Msemaji wa jeshi la Ufaransa awali alisema shughuli hiyo ilitazamiwa kuepuka umwagikaji damu.

Msemaji wa Bw Bw Ouattara amesema pia wapiganaji wake walihusishwa katika juhudi hizo.

Siku ya Jumapili, helikopta za Umoja wa Mataifa na Ufaransa zilianza kuvishambulia vituo mbalimbali vya kijeshi na maghala ya silaha ya Bw Gbagbo ambayo yana silaha kali.