Tetemeko lingine la ardhi latokea Japan!

Raia wa Japan akiomboleza Haki miliki ya picha 1
Image caption Tetemeko lingine latokea huku Japan ikiendelea kuomboleza

Tetemeko lingine kubwa la ardhi limetokea nchini Japan, wakati nchi hiyo ilikuwa katika shughuli za kulikumbuka jana lililotokea mwezi mmoja ukiwa uliopita, tetemeko la ardhi ambalo lilisababisha tsunami, na kuliangamiza eneo la kaskazini mashariki mwa nchi.

Tetemeko la hivi karibuni lenye kipimo cha Richter 7.1, nguvu zake hasa zilisikika zaidi kusini mwa Fukushima, ambako kinu cha nuklia kiliharibiwa sana mwezi uliopita.

Wafanyikazi katika eneo hilo waliondolewa wakati huo.

Mapema, serikali ilikuwa imetangaza kwamba itapanua eneo ambalo litafikiriwa kuwa ni hatari Fukushima, na kuwaondoa raia ili kuepuka mionzi ya nuklia.

Awali, raia walinyamaza kimya kwa kipindi cha dakika moja, katika hali ya kuwakumbuka watu 13,000 walioangamia mwezi mmoja uliopita.