Besigye akamatwa Uganda

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda, Dk Kizza Bessigye, amekamatwa katika mji mkuu wa Kampala.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Besigye amewataka raia wa Uganda kupinga ongezeko la bei za bidhaa muhimu

Dk Besigye alikamatwa lna kubebwa kwa gari la polisi, alipokuwa akitembea kutoka nyumbani kuelekea kazini.

Dk Besigye alikuwa amewataka raia wa Uganda kutembea kutoka nyumbani hadi kazini, kama njia moja ya kupinga ongezeko kubwa la bei ya vyakula na mafuta.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala anasema kuna watu wengi waliokamatwa, ikiwa ni pamoja na wanasiasa wachache wa upinzani.