Soka ya Olympic Sudan kuikabili Misri

Sudan baada ya kuiondoa Ghana katika kufuzu kwa mashindano ya soka kwa wanaume katika michezo ya Olympic ya mwaka 2012, imezawadiwa kucheza mkondo wa pili dhidi ya Misri.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ratiba ya soka kwa Olympic yatolewa

Tanzania, ambao walifanikiwa kuwafunga Cameroon katika hatua ya mwisho, itakabiliana na washindi wa medali ya dhahabu mwaka 1996 Nigeria.

Congo Brazzaville inasubiri mshindi kati ya Liberia na Ivory Coast.

Mchezo ambao ulisogezwa mbele umepangwa kuchezwa mjini Monrovia tarehe 20 mwezi huu wa Aprili, huku wakiwa Ivory Coast wanaongoza mabao 4-0.

Washindi wanane baadae wataingia hatua ya mwisho ya kufuzu, utaratibu ambao bado haujaanza kutumika.

Nchi tatu za Afrika, zitafuzu kwa ajili ya michezo ya mwakani ya Olympics mjini London, ambapo nchi itakayoshika nafasi ya nne italazimika kucheza dhidi ya nchi moja ya Asia kutafuta nafasi ya kuwemo katika michezo hiyo.

Duru ya kwanza ya raundi ya pili itachezwa mwishoni mwa wiki kati ya tarehe 3-5 mwezi wa Juni na mechi za marudiano zitakuwa wiki mbili baadae.

Ratiba ya Raundi ya pili ni hii ifuatayo:

Algeria v Zambia

Morocco v Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo

Congo v Ivory Coast au Liberia

Gabon v Mali

Sudan v Misri

Benin v Afrika Kusini

Tunisia v Senegal

Tanzania v Nigeria