Huwezi kusikiliza tena

Niqab na Burka

Mavazi yanayofunika uso gubigubi-NIQAB au kuacha macho tu BURKA yamepigwa marufuku kuvaliwa hadharani nchini Ufaransa. Sheria inayozuia uvaaji huo ilianza kutumika rasmi wiki hii nchini humo. Wanawake wawili walitiwa nguvuni na baadaye kuachiliwa baada ya kuhusishwa na maandamano yasiyo rasmi yanayopinga sheria kuzuia mavazi hayo.

Ufaransa inakuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kupitisha sheria hiyo. Anayekamatwa analipishwa faini ya dola 133 au pound 217. Wanaowalazimisha wanawake kuvaa mavazi hayo kufunika uso gubigubi au kubakisha macho tu wanakabiliwa na faini kubwa zaidi au kufungwa jela miaka miwili.

Sheria hiyo haijagusia mavazi mengine kama hijab -linalofunika kichwa tu na kuacha uso. Hijab ni neno la kiarab na vazi hili huvaliwa na wanawake wa kiislam na wengine kama ishara ya heshima kwa mwanamke kutoacha viungo vyake wazi.

Mjadala huu unazungumzia iwapo mavazi haya ya gubigubi -niqab au Burka inayoacha macho tu yazuiwe? Je ni utamaduni au yanahusihwa na masuala ya dini. Wachangiaji ni pamoja na :

Bi Mzuri Issa aliyeko Zanzibar, Tanzania, yeye ni mwandishi wa habari na mwanaharakati wa masuala ya wanawake

Bi Halima Shwaib aliyeko Dar es Salaam, Tanzania ni mwalimu , na anavaa Niqab

Sheikh Jongo, Imam wa msikiti wa Manyema - Dar es Salaam, Tanzania

Na pia

Adam Khamis Mwamburi, mwanafunzi wa Udaktari wa falsafa Ph.D -kutoka Taasisi ya Kimataifa ya masomo kuhusu mtazamo na ustaarabu katika Uislam nchini Malaysia

Haijat Habiba- anavaa niqab na anaishi Burundi