Nigeria: zoezi la kuhesabu kura laendelea

Shughuli za kuhesabu kura zinaendela nchini Nigeria ambapo mamilioni ya watu walipiga kura kumchagua rais Jumamosi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchaguzi Nigeria

Taarifa zinaonyesha kuwa idadi za kura kati ya wagombea wawili Rais Goodluck Jonatahan an Muhammadu Buhari zinakaribiana sana.

Ripoti za awali zilionyesha Bw Jonatahna akiongoza lakini pia zilionyesha Bw Buhari kuwa na kura nyingi katika maeneo ambayo ana ushawishi mkubwa.

Bw Jonathan, Mkristo kutoka jimbo la Niger Delta linalotoa mafuta, anaelekea kuwa na wafuasi wengi kusini mwa nchi.

Naye Jenerali Buhari anaongoza katika eneo la Waislamu wengi la kaskazini.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa katika siku mbili zijazo.

Wasimamizi wa kimataifa walisema uchaguzi huo unaweza kuwa ndio wa kuaminika kabisa kufanywa Nigeria katika miongo kadha; tofauti na chaguzi zilizopita ambapo kulitokea udanganyifu na ghasia.