Arsenal yabanwa, Chelsea yapeta

Chelsea imeiruka Arsenal katika msimamo wa ligi na kujikita katika nafasi ya pili baada ya kuichapa Birmingham kwa mabao 3-1.

Image caption Malouda na Drogba

Flourent Malouda aliandika bao la kwanza kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Didier Drogba, dakika tatu baada ya kuanza kwa mchezo.

Bao la pili lilifungwa na Salomon Kalou katika dakika ya 26.

Malouda alipachika bao lake la pili katika mchezo huo katika dakika ya 62, na kuipatia Chelsea mabao matatu.

Goli la Birmingham la kufutia machozi lilipatikana katika dakika ya 76, kwa mkwaju wa penati, uliofungwa na Sebastian Larsson.

Arsenal yatoka sare

Matumaini ya Arsenal kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England yaliingia dosari baada ya timu hiyo kutoka sare ya 3-3 na mahasimu wao wa kaskazini mwa London Tottenham Hotspur.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Van Der Vaart alifunga bao la penati

Katika mchezo uliokuwa wa kuvutia, Theo Walcott aliandika bao la kwanza la Arsenal, kabla ya Rafael Van Der Vaart kusawazisha.

Samir Nasri alipachika bao la pili la Arsenal, kabla ya Robin Van Persie kupachika goli la tatu.

Hata hivyo kabla ya mapumziko Tom Huddlestone alifunga bao la pili la Spurs.

Bao la kusawazisha la Spurs lilifungwa na Rafael Van Der Vaart kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha pili.

Chelsea imebakiza michezo mitano - ukiwemo dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford, Mey 8, huku Man U wenyewe wakiwa na mchezo dhidi ya Arsenal, kwenye uwanja wa Emirates.