Utaratibu wa harusi ya Kifalme

Kate Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kate na William

Taarifa zimetolewa kuhusu harusi ya Kifalme.

Usiku wa kuamkia siku ya harusi, Bi harusi, Kate Middleton na ndugu zake wa karibu watakaa katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano iitwayo Goring iliyopo eneo la Belgravia, katikati ya jiji la London.

Taarifa kutoka makazi ya kifalme ya jijini London, Clarence House pia imetoa muda wa utaratibu wa shughuli zitakavyokuwa siku hiyo, na hata njia ambayo maharusi watapita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maharusi, Kate na William

Wakati huohuo, mdogo wa bwana harusi, Mwana Mfalme Harry, ameungana na Bi harusi katika kufanya mazoezi ya siku hiyo kubwa, katika kanisa la Westminster Abbey.

Harry, atakuwa mpambe wa kaka yake siku ya harusi.

Mpambe wa Bi harusi, ni mdogo wake aitwaye Pippa Middleton.

Bwana Harusi,William, hajahudhuria shughuli za mazoezi ya harusi kwa sababu yuko kazini. William ni rubani wa helikopta za uokoaji.