Dr Besigye wa Uganda akamatwa tena

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Dr Kiiza Besigye

Kiongozi wa upinzani wa Uganda Kiiza Besigye amekamatwa karibu na nyumba yake baada ya kudhamiria kujiunga na maandamano mapya kupinga kupanda kwa gharama za maisha.

Wiki iliyopita pia alikamatwa kutokana na kampeni ya "kutembea kazini" kwa makundi na kupigwa risasi mkononi baada ya kuibuka ghasia baina ya polisi na wafuasi wake.

Viongozi wengine wa upinzani nao wamekamatwa kutokana na maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kila Jumatatu na Alhamis.

Mwishoni mwa juma, Rais alielezea mpango huo kuwa wa "kipumbavu" na kinyume cha sheria.

Dr Besigye alishindwa na matokeo yake Rais Yoweri Museveni aliibuka mshindi katika uchaguzi wa mwezi Februari huku akidai uchaguzi huo ulifanyiwa hila.

Ameshindwa mara tatu na Bw Museveni katika uchaguzi wa rais, akiwa ameongeza asilimia 26 zaidi ya asilimia 68 za rais huyo mwezi Februari.