Wafanyakazi wa kutoa misaada ruhsa Libya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mtoto aliyejeruhiwa Misrata

Kulingana na Umoja wa Mataifa, serikali ya Libya imeahidi kutoa ruhusa kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika maeneo inayodhibiti.

Maafisa wa umoja huo wamesema makubaliano hayo yanawaruhusu wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu kuwepo kwenye mji mkuu, Tripoli, na kuingia na kutoka wakati wowote nchini humo.

Wakati huo huo, takriban watu 1,000 walioondolewa kutoka Misrata wamewasili katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Benghazi.

Majeshi yanayomwuunga mkono Gaddafi yamekuwa yakishambulia Misrata kwa siku kadhaa sasa na mamia ya watu wanadhaniwa kufariki dunia.

Walioondolewa wamesafirishwa kwa kutumia meli iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la kutoa misaada la IOM, linalosema wengine kwa maelfu bado wanasubiri kuokolewa.