Arsenal yaboronga

Matumaini ya Arsenal kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England yamefifia zaidi baada ya kufungwa 2-1 na Bolton.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bolton

Arsenal wakicheza chini ya kiwango chao katika kipindi cha kwanza walifungwa na Daniel Sturridge kwa bao la kichwa kufuatia mpira wa kona.

Mapema katika kipindi cha pili, Kipa Wojciech Szczesny aliokoa mkwaju wa penati uliopigwa na Kevin Davies, na dakika moja baadaye Robin Van Persie kufunga bao la kusawazisha kwa Arsenal.

Arsenal walikuwa na nafasi za kutosha kushinda mchezo huo, lakini walijikuta wakipoteza katika dakika ya mwisho.

Tamir Cohen aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona na kuwapa ushindi Bolton.

Arsenal walitakiwa kupata ushindi katika mchezo huu ili kuwa na matumaini ya kuwania ubingwa.