Polisi Uchina wawatia waumini kizuizini

Polisi wa Uchina wamewatia kizuizini wafuasi wa kanisa liliopigwa marufuku la Shouwang.

Image caption Pasaka

Watu hao wasiopungua 20 walikamatwa walipokuwa wakifanya mhadhara wa pasaka wakiwa nje.

Kanisa hilo la ki-evangelisti lina wafuasi takriban elfu moja katika mji mkuu wa Beijing.

Viongozi kutoka kanisa hilo wamepewa kifungo cha nyumbani, na wafuasi wa kanisa hilo pia wamekuwa wakikamatwa katika majuma ya hivi karibuni, katika juhudi za serikali kuangamiza upinzani.

Katiba ya Uchina inawapa watu uhuru wa kufanya ibada,lakini Wakristo takriban 70,000,000 ni wafuasi wa makanisa yaliyopigwa marufuku.