Mugabe amekaidi vikwazo na yuko Rome

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili mjini Rome, kushiriki kwenye sherehe za kuanzisha utaratibu wa kumtakasa Papa John Paul wa pili, hapo kesho.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Vikwazo vya Umoja wa Ulaya vinamkataza Bwana Mugabe kuzuru nchi zanachama.

Katika safari zake nyengine za kwenda Vatikani, alisema anapita njia tu mjini Rome.

Rais Mugabe, ambaye ni mkatoliki, ameshutumiwa kuwa amevunja haki za kibinaadamu nchini mwake.

Alipohojiwa na BBC Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Utaliana, Franco Frattini, alisema ingawa hawakufurahi, lakini hawawezi kumzuwia Rais Mugabe kwa sababu Vatikani ni taifa huru:

"Laa isingewezekana, kwa sababu ni kama Umoja wa Mataifa.

Madikteta wakiingia New York, Marekani haiwezi kuwazuwia.

Na hapa ni hivo hivo.

Ni Vatikani inayoandaa shughuli hii; na sisi tunaheshimu kikamilifu itifaki ya Vatikani".