Papa asema dipolmasia itumiwe Libya

Papa Benedict ametoa wito kuwa zitumike njia za kidiplomasia na mazungumzo kumaliza vita vya Libya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa Benedict

Piaa ameomba kuwa msaada upelekwe kwa wale wanaohitaji.

Papa alikuwa akiongoza ibada ya Jumapili ya Pasaka iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini wa kikatoliki katika medani ya St Peter's Vatikani.

Kuhusu Mashariki ya Kati kwa jumla alisema anatumai amani itatawala na kushinda magawanyiko, chuki na chuki na ghasia.

Papa pia alisihi umoja na wakimbizi wanaotoroka fujo, hasa kutoka nchi za Afrika.