Wanaharakati wakamatwa Syria

Taarifa kutoka Syria zinaeleza kuwa wanaharakati kadha wanaopinga serikali wamekamatwa baada ya maandamano ya Ijumaa na Jumamosi, ambapo watu zaidi ya mia moja waliuwawa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji Syria

Shirika la kuchunguza haki za kibinaadamu la Syria limelaani kukamatwa kwa watu hao na kutaka waachiliwe huru.

Hakuna njia ya kuthibitisha habari hizo.

Hapo awali, wakuu wa Uingereza iliwasihi raia wake wote walioko Syria waondoke kwa sababu hali ya usalama inazidi kuwa mbaya.