Cambodia na Thailand katika mapigano

Mapigano yameandelea leo kwa siku ya tatu mfululizo baina ya majeshi ya Thailand na Cambodia kwenye mpaka wao.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mjeruhi akihamishwa

Mwandishi wa BBC anasema kila upande unazidi kutoa matamshi ya hamasahuku Cambodia inaishutumu Thailand kuwa inatumia gesi ya sumu; na Thailand kudai kuwa Cambodia inatumia wanawake na watoto kama ngao.

Katika hotuba yake ya kila juma, Waziri Mkuu wa Thailand, Abhisit Vejja-jiva, aliilaumu Cambodia kuwa ndiyo iliyoanza uchokozi.

"Kwa siku mbili sasa, pamekuwa mapambano karibu na mahekalu ya Ta Muan na Ta Kwai, ambayo yako katika majimbo ya Surin na Buriram.

Leo asubuhi pia kumetokea mapambano hapa na pale.

Napenda kukariri msimamo wa Thailand, kwamba sisi hatuna azma ya kumteka au kumshambulia yeyote.

Ni wajibu wetu kulinda uhuru wetu kikamilifu.

Hili tukio linatokana na hatua iliyoanzishwa na Cambodian."