Besigye bado hakupona macho

Taarifa kutoka Kenya zinasema kiongozi wa upinzani, Doctor Kizza Besigye, ambaye anauguzwa hospitali mjini Nairobi, bado hawezi kuona, baada ya kurushiwa pili pili kwenye macho, wakati wa maandamano ya upinzani.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Watu wawili waliuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa kwenye ghasia mjini Kampala, siku ya Ijumaa, baada ya mwanasiasa huyo kukamatwa.

Viongozi wa kidini wameshauri kuwa kufanywe mazungumzo baina ya serikali na upinzani wakati fujo za kisiasa nchini Uganda zinazidi kuwa mbaya.

Na Waziri wa Habari wa Uganda, Kabakumba Matsiko, aliiambia BBC kwamba maandamano hayataruhusiwa kuendelea.