Makubaliano yamefikiwa Yemen

Chama tawala cha Yemen kimekubali pendekezo la nchi za Ghuba, kwamba Rais Ali Abdullah Saleh aondoke madarakani, kwa shuruti kuwa hatoshtakiwa.

Haki miliki ya picha Reuters

Mpango huo unatarajiwa kumaliza maandamano yaliyoendelea kwa miezi kadha.

Mpango unapendekeza kuwa rais akabidhi madaraka kwa naibu wake katika muda wa siku 30, baada ya maridhio ya upinzani.

Muungano wa vyama saba vya upinzani ulikaribisha mpango huo, lakini unaona kuna mushkili.

Wao wanataka Rais Saleh aondoke madarakani kabla ya kuunda serikali ya kuunganisha taifa.

Marekani imezisifu pande zote mbili kwa kukubali pendekezo hilo, na imetoa wito kuwa madaraka yakabidhiwe kwa uongozi mpya kwa haraka na kwa amani.