Nigeria yachagua magavana

Image caption Upigaji kura Nigeria

Raia wa Nigeria wanapiga kura katika duru ya mwisho katika mchakato mrefu wa uchaguzi uliojaa vurugu.

Uchaguzi wa magavana 36 wenye ushawishi mkubwa umecheleweshwa katika majimbo mawili yaliyoathirika zaidi na ghasia.

Mabomu mengi zaidi yamelipuka kwenye mji wa Maiduguri kaskazini-mashariki mwa mji huo, ambapo takriban watu watatu waliuawa tangu siku ya Jumapili.

Shirika la kutetea haki za bindamu la Nigeria limesema zaidi ya watu 500 walikufa kufuatia ghasia ziliozibuka baada ya uchaguzi wa rais.

Ghasia ziliibuka upande wa kaskazini baada ya Bw Goodluck Jonathan, mkristo kutoka kusini, alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Aprili 16.

Makanisa yalichomwa moto na Waislamu walilengwa katika mashambulio ya kulipiza kisasi.

Wakristo wengi walisherehekea sikukuu ya Pasaka kwenye kambi za jeshi ambapo walijihifadhi kutokana na vurugu hizo.

Licha ya kuwepo ghasia, waangalizi wengi walisema uchaguzi umekuwa bora zaidi tangu kurejeshwa kwa uongozi wa kiraia mwaka 1999.