Besigye kufikishwa mahakamani leo-Kampala

Besigye Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Besigye

Kiongozi wa chama cha Forum for democratic Change FDC, nchini Uganda, Dr Kizza Besigye anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kusikia ombi lake la kupewa dhamana baada ya kukamatwa wiki iliopita.

Dr Besigye ameshtakiwa kwa kosa la kufanya mkutano kinyume na sheria.

Hii ni baada ya jaribio lake la kufanya mgomo wa kususia usafari wa magari kufuatia kuogezeka kwa bei ya petroli.

Kiongozi huyo alinyimwa dhamana na kupelekwa rumande katika gereza la Nakasongola mjini Kampala.