Bunge kujadili ongezeko la bei ya chakula-Kenya

Raia wa Kenya wakiandamana kupinga bei ya Petroli Haki miliki ya picha other
Image caption Raia wa Kenya wakiandamana kupinga bei ya Petroli

Nchini Kenya, Waziri mkuu Raila Odinga, leo anatarajiwa kufafanua bungeni hatua serikali inachukua kudhibiti hali.

Wiki iliopita shirika linalotetea haki za wanunuzi liliandaa maandamano katika sehemu kadhaa nchini, kulaani ongezeko hilo.

Chama cha wafanyikazi kimetisha kuongoza mgomo tarehe mosi mwezi Mei mwaka huu, ikiwa mishahara ya wafanyikazi haitaongezwa, suala linalozua wasi wasi serikalini na miongoni mwa wawekezaji.