Maafisa wa polisi wapya wasajiliwa Kenya

Mkuu a Polisi nchini Kenya Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mkuu a Polisi nchini Kenya

Usajili wa makurutu watakao jiunga na kikosi polisi nchini Kenya umekamilika huku mabadiliko makubwa yakishuhudiwa ili kuhakikisha kuwepo na uwazi katika utekelezaji wa mchakato mzima.

Makurutu elfu saba walitarajiwa kusajiliwa kutoka wilaya 47 kote nchini na kujiunga na vikosi vya polisi tawala na polisi wa kawaida.

Ili kuhakisha kuwepo kwa uwazi na usawa katika usajili huo, wasajili waliweka mikakati kadhaa ili kupunguza visa vya ufisadi au ukiukaji wa sheria katika usajili wa makuruti.