Matokeo ya mechi za EPL Jumamosi

Wigan imeshinda kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 1-1 na Everton.

Wigan walipata bao lao kupitia Charles Nzogbia, lakini Hugo Rodallega aliunawa mpira ndani ya eneo la hatari na kusababisha penati.

Leighton Baines alipiga mkwaju wa penati na kusawazisha bao kwa Everton.

Wigan walihitaji ushindi ili kuwa na matumaini ya kutoshuka daraka.

Katika michezo mingine Blackbur imeichapa Bolton 1-0, Blackpool imetoka sare ya 0-0 na Stoke City.

Sunderland imechapwa 3-0 na Fulham, huku West Brom nayo ikiizaba Aston Villa 2-1.