Wakili achukulwia hatua na ICTR

Mauaji ya rwanda
Image caption Mauaji ya rwanda

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda-ICTR imemchukulia hatua wakili wa Kimarekani Peter Erlinder baada ya kukataa kushiriki kwenye kesi hiyo akihofia usalama wake.

Mahakama hiyo imemuondoa kwenye wadhifa wake wakumtetea Meja Aloys Ntabakuze, anayetuhumiwa kuhusika katika mauaji hayo.

Mahakama hiyo inasema hatua ya Wakili Erlinder ya kukataa kushiriki katika kesi hiyo ni sawa na kukaidi sheria za mahakama hiyo.

Itakumbukwa pia wakili hiyo alifunguliwa mashataka na serikali ya Rwanda ya kukana mauaji ya Kimbari mwaka uliopita alienda kumwakilisha mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire aliyekuwa akigombea urais wa nchi hiyo.