Hayati Papa John Paul anatukuzwa

Waumini wengi wa Kikatoliki kutoka sehemu mbali mbali za dunia walikusanyika medani ya St Peter's mjini Rome, kwa sherehe ya kufwata utaratibu wa kumtukuza hayati Papa John Paul wa Pili.

Haki miliki ya picha Reuters

Viongozi wa nchi 16 piya walihudhuria.

Mwandishi wa BBC mjini Rome, anasema inakisiwa kuwa watu zaidi ya milioni moja wamehudhuria sherehe hiyo, na kupiga makofi wakati picha ya hayati Papa John Paul ilipofunuliwa, na kuoneshwa kwenye medani ya St Peters.

Papa Benedict, alitangaza kuwa aliyemtangulia, ambaye alifariki mwaka wa 2005, kuwa Mkatoliki "aliyebarikiwa", hatua ya mwisho kabla ya kufikia cheo cha kutakasika.