Vifaru vinaingia Banias, Syria

Taarifa kutoka Syria zinaeleza kuwa vifaru vimepelekwa katika mji wa bandari wa Banias, ambao umekuwa na maandamano kadha dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Ripoti zinasema vifaru vinaelekea maeneo ya watu wa madhehebu ya Sunni, lakini siyo ya Alawi, koo za Kishia anakotoka Rais Assad.

Mwandishi wa BBC anasema ripoti hizo zikithibitishwa, basi ni tukio la hatari, kwa sababu linaweza kuleta mgawanyiko kati ya madhehebu tofauti.

Siku ya Ijumaa watu zaidi ya 20 waliuliwa na askari wa usalama, wakati wa maandamano dhidi ya serikali nchini Syria.

Marekani imeonya kuwa itachukua hatua zaidi dhidi ya Syria iwapo serikali ya Rais Assad itashindwa kuacha kukandamiza waandamanaji kwa nguvu.

Lakini Marekani haikueleza itachukua hatua za namna gani.