Umoja wa Mataifa unaisihi Uganda

Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na haki za kibinaadamu, Navi Pillay, ameisihi Uganda kuacha kutumia kile alichokielezea kuwa nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji wa upinzani.

Haki miliki ya picha AP

Bibi Pillay alisema hatua za wakuu wa Uganda ndio sababu kubwa iliyogeuza maandamano ya amani kuwa msuko-suko wa kitaifa, ambapo watu kama wanane waliuwawa.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa alisema aliyotendewa kiongozi wa upinzani, Dakta Kizza Besigye, yameshtuwa.

Bwana Besigye bado hawezi kuona sawa sawa, baada ya kurushiwa pilipili machoni, na polisi wa Uganda.

Maandamano mengine ya kupinga kuzidi kwa gharama za maisha, yanapangwa kufanywa Jumatatu.