Obama: Dunia salama pasipo bin Laden

Rais Barack Obama wa Marekani amekielezea kifo cha kiongozi wa al-Qaeda, Osama Bin Laden, kuwa ni "siku njema kwa taifa la Marekani," na kusema sasa dunia imekuwa mahala salama na pazuri zaidi.

Haki miliki ya picha other
Image caption Nyumba ambako Osama bin Laden alikutwa na kuuawa huko Pakistan.

Bin Laden aliuawa katika shambulio lililofanywa na vikosi maalum vya Marekani kwenye nyumba moja ndani ya mji wa Abbottabad nchini Pakistan.

Anaaminika kuwa ndiye mtu aliyeagizwa kufanyika kwa mashambulio yaliyotokea New York na Washington, Septemba 11 mwaka 2001, pamoja na mashambulio mengi kadhaa ya mabomu yaliyosababisha vifo.

Alikuwa ndiye mtu anayesakwa zaidi duniani.

Lakini maelezo yake katika orodha hiyo yamebadilishwa na sasa kuna sehemu inasomeka: "Amefariki".

Uhakika

Vipimo vya DNA vilivyofanywa baada ya harakati hiyo vinaonyesha kwa uhakika wa asilimia "99.9%" kuwa mtu aliyepigwa risasi ni Osama Bin Laden, maafisa wa Marekani walieleza.

Maafisa wa wizara ya ulinzi wanaeleza kuwa alizikwa baharini baada ya kuswaliwa kwa mujibu wa taratibu za kiislamu kwenye meli ya kubebe ndege katika bahari ya Arabuni.

Marekani imeweka ofisi zake katika hali ya tahadhari kote duniani, ikiwaonya raia wake kuhusu uwezekano wa mashambulio ya al-Qaeda kulipiza kisasi kwa kifo cha Bin Laden.

Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la CIA, Leon Panetta, amesema al-Qaeda kuna uwezekano mkubwa kujaribu kulipiza kwa yaliyotokea.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii