Mawakili kuandamana Uganda:

Kizza Besigye kiongozi wa Upinzani Haki miliki ya picha BBC World Service

Mawakili nchini Uganda hii leo asubuhi wanapanga kufanya maandamano kupinga kile wanachosema ni ukiukaji wa sheria na serikali. Hii wanasema imejitokeza wazi katika kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kukabiliana na waandamanaji.

Katika kipindi cha karibu mwezi mmoja viongozi wa upinzani wamekuwa wakifanya maandamano ya kutembea kwa miguu kwenda kazini kuishinikiza serikali kupunguza gharama ya juu ya maisha.

Lakini serikali imepiga marufuku maandamano hayo huku polisi na jeshi wakiwapiga na kuwakamata mamia ya waandamanaji wakiwemo viongozi wa upinzani .

Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Uganda Dkt, Kizza Besigye amelazwa katika hospitali mmoja nchini Kenya baada ya kujeruhiwa na polisi walipokuwa wakimkamata.