Papa anataka waumini kupokea wakimbizi

Papa Benedict amewaomba Wakatoliki wa Utaliana wawe wavumilivu kwa wakimbizi kutoka Afrika Kaskazini.

Haki miliki ya picha Getty

Aliwaambia waumini katika mji mmoja wenye bandari, kwamba Wakatoliki wanafaa kuwakaribisha na kuwa karimu kwa maelfu ya wageni wanaowasili kwenye bandari zao mwaka huu.

Idadi ya wakimbizi kutoka Afrika Kaskazini imezidi kwa sababu ya ghasia katika nchi za eneo hilo.

Jana usiku meli ya wavuvi, iliyobeba mamia ya watu kutoka Libya, iligonga mwamba ilipojaribu kutia nanga katika kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa.

Taarifa zinasema abiria wote walinusurika, na wengine walisaidiwa na walinzi wa pwani wa Utaliana.