Vifaru vimepelekwa Homs, Syria

Askari wa usalama wa Syria wamepeleka vifaru katika mitaa ya kati-kati ya mji wa Homs, na kuna ripoti kuwa baadhi ya watu wamekamatwa na risasi zimefyatuliwa.

Haki miliki ya picha Reuters

Televisheni ya taifa ya Syria imetangaza kuwa wachochezi waliokuwa na silaha wameuwawa, na baruti imechukuliwa na serikali.

Operesheni za jeshi la usalama piya zimeendelea katika mji wa Banias, ulio kando ya bahari, na kwenye mji wa Deraa uliozingirwa, kusini mwa nchi.

Mji wa Deraa ndio umeshuhudia ghasia kubwa kabisa, tangu maandamano kuanza zaidi ya mwezi mmoja uliopita.