Waasi wawatimua wanajeshi Libya

Mpiganaji wa waasi mjini Misrata Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mpiganaji wa waasi mjini Misrata

Waasi katika mji wa Libya wa Misrata wamesema kuwa wamewatimua wanajeshi wa serikali hadi nje ya mji huo.

Misrata ndio mji pekee magharibi mwa Libya ambao unadhibitiwa na waasi hao na umekuwa ukishambuliwa na majeshi yanayomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi kwa muda wa miezi miwili.

Waasi na raia wamekuwa wakishambuliwa na majeshi ya Gaddafi.

Mkuu wa huduma za misaada wa umoja wa mataifa ameamuru kusitishwa kwa mashambulizi hayo ili kupunguza hatari kwa raia na kuelezea hali mjini Misrata kuwa mbaya zaidi.

Katibu msaidizi anayeshughulikia misaada kwa raia,amesema ''Wasiwasi wetu mkubwa ni mjini Misrata,mashambulizi na mapigano yamekuwa yakiendelea katika sehemu za mji huo kwa zaidi ya miezi miwili.Bidhaa ziko,lakini wtu wengine sasa hawana chakula ,maji na bidhaa zengine muhimu.''

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Valarie Amos

Waasi wanasema kuwa mji huo bado umezungukwa,lakini kwa sasa wameweza wamesogea hadi kilomita thelathini magharibi mwa mji wa Tripoli.

Shirika la habari la serikali limesema kuwa ndege ya shirika la NATO ilishambulia wanajeshi na raia katika miji ya Misrata na mji wa karibu wa Zlitan.

Kutokana na vikwazo vya kupata taarifa kutoka nchi hio imefanya kuwa vigumu kuthibitisha taarifa hizo.