Watu 80 wauawa Sudan Kusini

Wanjeshi wa SPLA Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanjeshi wa SPLA

Watu wasiopungua themanini wameuawa katika eneo la Sudan kusini baada ya waasi kuvamia kambi za mifugo, jeshi la Sudan kusini limesema.

Wavamizi hao waliwauwa watu 34 wakiwemo wanawake na watoto, wakati walipoiba mifugo katika jimbo la Warrap, amesema msemaji wa jeshi Philip Aguer.

Lakini wakati wakitoweka na mifugo, wezi hao walishambuliwa na 48 kati yao kuuwawa.

Sudan kusini inajitenga na eneo la kaskazini mwezi Julai mwaka huu. Sudan Kusini inaishutumu Khartoum kwa kusababisha hali ya wasiwasi katika eneo hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Sudan

Madai kama hayo yamepingwa na serikali ya Rais Omar al-Bashir.

Umoja wa mataifa umesema kuwa makundi yasiyopungua saba ya wapiganaji waliojihami yanaendesha shughuli zake Sudan Kusini.

Umoja wa mataifa unakadiria kwamba zaidi ya watu 1,000 wameuawa mwaka huu katika mapigano kati ya waasi au makundi yaliyojihami na jeshi la Sudan Kusini.

Jamii nyingi za eneo la Sudan Kusini pamoja na mataifa jirani hutegemea sana mifugo kwa maisha yao.