Huwezi kusikiliza tena

Ardhi yazua kizaazaa Tanzania

Kumetokea tafrani baada ya watu wanaodaiwa kuwa wanajeshi kutoka Kambi ya Kunduchi nchini Tanzania kuvamia makazi ya watu na kuwapiga na kisha kuwazuia kwa muda kwenye kambi hiyo huku wakiwaadhibu kijeshi, kwa madai ya kuingilia eneo linalomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Watu wawili akiwemo mama mjamzito wamelazwa Hospitali ya Muhimbili kutokana na tukio hilo. Pia kumekuwa na ripoti za uporaji wa mali. Mwandishi wetu wa Dar es salaam Erick David Nampesya ametutumia taarifa zaidi.