Wakongomani wafikishwa mahakamani Kenya

Raia watatu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamefikishwa mahakamani nchini Kenya, baada ya kukamatwa wakisafirisha zaidi ya 400 za dhahabu.

Image caption Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa ikipoteza dhahabu kutokana na biashara ya magendo

Mwanadiplomasia wa Congo, Bob Katamba, alisema serikali yake inaamini kwamba mshukiwa mmoja, Jean-Claude Mudeke Kabamba, alikuwa ndiye kiongozi wa kundi moja la wafanya biashara za magendo, na vile vile kundi moja linalomiliki silaha kinyume na sheria, mashariki mwa Congo.

Watu hao wamo katika orodha ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ya wafanya magendo wakubwa zaidi wa dhahabu, ambao katika miezi michache iliyopita, waliweza kuuza zaidi ya tani mbili unusu za dhahabu kutoka nchi hiyo.