Maisha mafupi kusini mwa Afrika

Takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa, kwa sababu ya UKIMWI kusini mwa Afrika, urefu wa wastani wa maisha ya Muafrika Kusini umepungua kwa miaka 9, na miaka 12 Swaziland na Zimbabwe, ikilinganishwa na mwaka 1990.

Lakini watu wanaishi kwa muda mrefu zaidi katika nchi nyengine za Afrika na dunia.

Eneo la kusini mwa Afrika ndilo liloathirika vibaya kabisa na UKIMWI katika bara hilo.