Blackpool, Wolves na West Brom zashinda

Blackpool imeweka hai matumaini ya kutoshuka daraja baada ya ushindi mnono wa mabao 4-3 dhidi ya Bolton katika mchezo uliokuwa wa vuta nikuvute.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption DJ Campbell

Kevin Davies wa Bolton alikuwa wa kwanza kuipatia timu yake bao mapema dakika ya sita, lakini dakika tatu baadae DJ Campbell aliisawazishia Wolves na dakika kumi baadae Jason Puncheon akaandika bao la pili kwa mkwaju wa yadi 18.

Matt Taylor aliisawazishia Bolton na alikuwa kwa mara nyingine Campbell aliyeandika bao la tatu kwa Wolves kabla ya mapumziko.

Daniel Sturridge aliisawazishia Bolton na kufanya ubao wa mabao uoneshe 3-3, lakini Charlie Adam akakamilisha kazi kwa kupachika bao la ushindi la nne kwa Wolves..

Kwa matokeo hayo, Blackpool wanaendelea kubakia nafasi tatu kutoka chini wakiwa na pointi 39, lakini timu nne zilizo juu yake kimahesabu zinaweza nazo kuporomoka na kushuka daraja.

Wolves nayo imepata ushindi muhimu katika hekaheka zao za kuwania kubakia Ligi Kuu ya England msimu ujao, baada ya kuilaza Sunderland ugenini kwa mabao 3-1.

Image caption Charlie Adam

Ushindi huo umeifanya Wolves kufikisha pointi 40 wakiwa nafasi ya 16, nafasi mbili tu chini ya timu tatu zilizo mstari wa kuteremka daraja.

Huo unakuwa wa kwanza kwa meneja Mick McCarthy katika uwanja wa Stadium of Light akiwa meneja katika timu ya Ligi Kuu ya England.

Bao la Youssouf Mulumbu katika dakika ya10 liliihakikishia ushindi mzuri West Brom kumaliza mechi zao za Ligi katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Everton waliocheza pungufu ya mchezaji mmoja.

Image caption Youssouf Mulumbu

Mulumbu alifunga kwa mkwaju wa karibu na lango baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Peter Odemwingie kufuatia krosi safi iliyochongwa na Chris Brunt.

Victor Anichebe, Johnny Heitinga na Leon Osman wote walikaribia kuipatia bao Everton, lakini tatizo lao la kufunga liliongezwa zaidi baada ya Diniyar Bilyaletdinov aliyeingizwa kipindi cha pili, kutolewa kwa kadi nyekundu.

Bilyaletdinov alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea vibaya James Morrison.

Matokeo hayo yameifikisha West Brom nafasi ya 10 wakiwa na pointi 46, huku Everton wakiwa nafasi ya saba na pointi 51.